Loading...
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameonyesha kuwa na hofu na mustakabali wa Umoja wa Ulaya.
Akihutubia katika bunge la EU Strasbourg Macron ameonyesha wasiwasi wake wa kuwepo kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya nchi za Umoja wa Ulaya.
Ameitaka EU kuchukua hatua muhimu kuhusiana na suala hilo.
"Sio raia wanaoutelekeza Umoja wa Ulaya bali ni viongozi wenyewe",alisema Macron.
Macron anaamini huu ndio muda muafaka wa Ulaya kulishughulikia suala hilo.
Na Geofrey Okechi.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za ulimwenguni punde zinapojiri.
"ULAYA YAGAWANYIKA"
Reviewed by By News Reporter
on
4/18/2018 01:52:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: