Loading...

ZARI ANUNUA MERCEDES YA KIFAHARI MIEZI KADHAA BAADA YA KUACHANA NA DIAMOND

Loading...
Mpenzi wa zamani wa Diamond Platinumz, Zari alitangaza kupitia mtandao wa Instagram kuwa alikuwa na pesa nyingi na kuamua kununua gari nyingine la kifahari lenye mtoko wa kipekee.

Zari alisema kuwa kwa alifanya kazi kwa bidii basi aliamua kujipatia zawadi ya kipekee.

Zari alisema pia ameajiri dereva mpya na amenunua gari mpya.

Mama huyo wa watoto watano amejulikana kwa kupenda vitu vizuri sana katika maisha yake, na mwaka jana alitangaza kwa mashabiki wake aliponunua gari mpya.

Zari amenunua gari hiyo aina ya Mercedes miezi kadhaa baada ya kutengana na Diamond Platinumz.

Kabla ya kutengana na Diamond Platinumz, Zari alikuwa tayari amenunua majumba kadhaa ya kifahari nchini Afrika Kusini na Uganda. Pia wapenzi hao walikuwa na nyumba nyingine Tanzania.

Kutengana kwake na Diamond kumempa raha zaidi, anaonekana kusafiri sana na kutumia pesa nyingi kupata mavazi na viatu kutoka kwa wanamitindo wa hadhi ya juu duniani.
Na Neema Joshua.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
ZARI ANUNUA MERCEDES YA KIFAHARI MIEZI KADHAA BAADA YA KUACHANA NA DIAMOND ZARI ANUNUA MERCEDES YA KIFAHARI MIEZI KADHAA BAADA YA KUACHANA NA DIAMOND Reviewed by By News Reporter on 4/14/2018 06:41:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.