Loading...

AFUNGWA MIAKA 25 JELA KWA KUWAAMBUKIZA WATU 200 UKIMWI

Daktari feki aliyewaambukiza wagonjwa 200 virusi vya ukimwi nchini Cambodia amehukumiwa jela. Daktari huyo bandia alipatikana na hatia ya kuwaambukiza takriban watu 200 virusi vya ugonjwa wa Ukimwi amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa makosa yake.

Baadhi ya wahathiriwa wa makosa hayo wamekwisha fariki dunia, Yem Chrin alikuwa akitumia sindano zilizokuwa zimekwisha tumika kuwatibu wenyeji wa kijiji cha Roka bila ya kujua alikuwa akisambaza Virusi vya Ukimwi. Awali Chrin alikuwa ameshtakiwa kwa mauaji lakini upande wa mashta
Loading...
a ukabadilisha shtaka na kuwa kuua bila ya kukusudia.

Kesi hiyo imefichua uhaba wa madaktari na ugumu ulioko kwa raia kupata huduma za afya katika maeneo mengi ya vijijini nchini Cambodia.

Utafiti umebaini kuwa zahanati nyingi katika maeneo ya vijijini huendeshwa na madakatari bandia ambao hawajahitimu kuwatibu wagonjwa.
Na Hamisi Fakhi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
AFUNGWA MIAKA 25 JELA KWA KUWAAMBUKIZA WATU 200 UKIMWI AFUNGWA MIAKA 25 JELA KWA KUWAAMBUKIZA WATU 200 UKIMWI Reviewed by By News Reporter on 5/06/2018 08:40:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.