Loading...

ALIKIBA ATAJA JINA LAKE HALISI, KUMBE 'KIBA' SIO JINA LAKE

Loading...
Watu wengi wamekuwa wakijua kuwa jina la kiba ni jina la ukoo la familia hiyo na hii yote ni kutokana na kwamba ndio  ilivyozoeleka kwa sababu familia yote na ndugu wa karibu wa ali wamekuwa wakitumia jina hilo kama ndio jina la ukoo na kumbe sio kweli kuhusu hilo.

Kwa mara ya kwanza msanii ali kiba amefunguka asili ya jina lake hilo lakini pia amesema kwa nini na wapi lilitokea jina la alikiba kama watu walivyozea kumuita,Alikiba nasema kuwa jina lake halisi kabisa ni Ali Saleh Gentamilan lakini jina la kiba lilitokea kutokana na utani waliokuwa wakimtania mama yake kipindi cha ujauzito wake.

Alikiba anaelezea kuwa kipindi mama yake mzazi akiwa na mimba alikuwa akipenda kubana nguo zake na  vibanio na ndipo walipoanza kumwita mama vibanio na alipozaliwa yeye akapewa jina la kibanio na ndipo lilipotokea jina la 'kiba' ikiwa ni kifupi cha kibanio.

Hata hivyo jina hilo lilizoeleka kutoka utoto kwake na wadogo zake na ndio aliona liwe jina lake la usanii kitu mbacho limechukua familia yote na kuwa kama jinala ukoo.
Na Hamisi Fakhi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
ALIKIBA ATAJA JINA LAKE HALISI, KUMBE 'KIBA' SIO JINA LAKE ALIKIBA ATAJA JINA LAKE HALISI, KUMBE 'KIBA' SIO JINA LAKE Reviewed by By News Reporter on 5/21/2018 12:45:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.