Loading...
Shirika la umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limesema kuwa makundi yenye silaha nchini Sudan Kusini yamewaachia watoto zaidi ya 200 ambao walikuwa wanatumikishwa kama wapiganaji.
Inakadiriwa kuwa watoto zaidi ya elfu 19 bado wanapigana kwenye makundi mbalimbali nchini humo.
Kuachiwa kwa watoto 210 kunafanya idadi ya watoto walioachiwa ndani ya mwaka huu peke yake kutoka kwenye makundi hayo kufikia 806, amesema msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa unatarajia watoto zaidi kuachiwa siku za usoni ambapo jumla ya watoto elfu moja wataachiwa na makundi ya wapiganaji.
Farhan Haq amesema kuwa wengi wa watoto walioachiwa wanatoka kundi la waasi wa SPLM-IO huku 8 wakitoka kwenye jeshi la taifa la ukombizi.
Hata hivyo Umoja wa Mataifa umelaani kunyanyaswa kwa wafanyakazi wa mashirika ya misaada nchini Sudan Kusini, UN ikisema vurugu na vitendo vya kikatili vimezuia kufika kwa misaada ya kibinadamu kwa zaidi ya watu milioni 7.
Umoja wa Mataifa unasema jumla ya wafanyakazi wanne wameuawa na wengine 10 walitekwa nyara katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, huku ukisema upinzani na Serikali hawajafanya vyakutosha kusitisha mapigano na kuingilia kazi za wafanyakazi wa misaada.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

ASKARI WATOTO 200 WAACHIWA HURU KUTOKA MAKUNDI YA WAASI SUDANI KUSINI
Reviewed by By News Reporter
on
5/21/2018 03:27:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: