Loading...

BEI YA PETROL NA DIZELI YASHUKA, MAFUTA YA TAA YAPAA

Loading...
Watumiaji magari, mashine na mitambo inayotumia petroli na dizeli wapata ahueni baada ya bei ya bidhaa hizo kupungua, huku bei ya mafuta ya taa ikapanda.

Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Mafuta na Maji (Ewura), jana ilitangaza kushuka kwa bei ya Petroli na Dizeli kwa asilimia 2.7 na asilimia 3.8; na ongezeko la asilimia 0.09 kwa mafuta ya taa.

Taarifa iliyotolewa na Kaiumu Mkuu mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Nzingagwa Mchany ilisema bei hizo mpya zitatumika Tanzania Bara kuanzia leo.

Hata hivyo, kwa watumiaji wa mafuta yanayopitia katika Bandari ya Dar es salaam ni neema, lakini wa Bandari ya Tanga bei imeongezeka.

Mchany alisema mabadiliko hayo yanatokana na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na marekebisho ya bei yaliyofanywa na Ewura kutokana na kubadilika kwa tozo za wakala na Serikali za mitaa katika bidhaa hizo.

Ikilinganishwa na tangazo la bei ya mafuta la Aprili 4 kwa mafuta yanayopitia katika Bandari ya Dar es salaam, bei ya petroli imepungua kwa sh88 kwa lita (asilimia 3.8) na dizeli sh61 kwa lita(asilimia2.75); huku bei ya mafuta ya taa ikiongezeka kwa sh2 kwa lita sawa na asilimia 0.09.

Tofauti na wanunuzi wa rejareja, bei ya wale wa jumla upande wa petrol imepungua kwa sh100.91 kwa lita (asilimia 4.58), dizeli sh73.71 kwa lita (asilimia 3.52) na mafuta ya taa sh10.49 kwa lita sawa na asilimia 0.51.

Mafuta yanayopitia Bandari ya Tanga bei kwa wanunuzi wa rejareja imeongezeka kwa asilimia 0.71 kwa dizeli. Lakini wauzaji wa jumla bei imepungua kwa asilimia 0.46 (sh9.8 kwa lita) kwa petroli na asilimia 0.1 (Sh1.9 kwa lita ) kwa dizeli.

"Hakuna uingizaji mpya wa mafuta uliofanyika nchini kupitia Bandari ya Tanga, lakini kutokana na mabadiliko ya bidhaa hizo tofauti na ilivyotangazwa Aprili 4," alisema Mchany na kuongeza: "Bei ya petroli itaongezeka kwa Sh3 kwa lita, huku dizeli ikiongezeka kwa S15 kwa lita."

Kutokana na kupungua kwa mafuta ya taa katika bandari ya Tanga, Ewura imewashauri watumiaji wa mikoa ya Nyanda za Juu kuchukua bidhaa hiyo katika Bandari ya Dar es Salaam kwa bei elekezi.

Taarifa ya Mchany inasisitiza kila kituo cha kuuzia mafuta kuchapisha bei kwenye mabango yanayoonekana bayana na kituo kutoa risiti za kielektroniki (EFD) kwa kila mauzo.
Na Paskali Joseph.




Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za biashara punde zinapojiri.
BEI YA PETROL NA DIZELI YASHUKA, MAFUTA YA TAA YAPAA BEI YA PETROL NA DIZELI YASHUKA, MAFUTA YA TAA YAPAA Reviewed by By News Reporter on 5/02/2018 12:46:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.