Loading...

CUF WAJIPANGA MKUTANO MKUU

Loading...
Naibu Mkurugenzi wa Mipango wa Chama cha Wananchi (CUF) Nassor Seif upande unaomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba, amesema wapo kwenye mchakato wa kufanya mkutano mkuu kwa ajili ya kupata viongozi wapya.

Seif alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na Gazeti moja hapa nchini baada ya kuulizwa kuhusu madai ya chama hicho upande wa Lipumba ambaye ni mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, kufanya mkutano mkuu huku kikikabiliwa na mvutano wa uongozi uliosababisha kufunguliwa kesi mahakamani.

Alisema CUF kupitia Baraza Kuu, wanachosubiri ni kukutana pamoja na kutoa taarifa rasmi ya kufanyika kwa mkutano huo.

Alipoulizwa kuhusu wajumbe watakaoshiriki mkutano huo alisema kila kitu kinakwenda vyema na kusisitiza wajumbe halali wapo.

“Wajumbe wa mkutano mkuu wa Taifa watakapopata taarifa ya wito wa mkutano wasisite kujitokeza kwa lengo la kutimiza haki yao ya kikatiba. “Sisi tunafanya haya kwa mujibu wa katiba ya chama na ndiyo maana tumekuwa tukibarikiwa kila hatua na wenye kujua ukweli sasa wameanza kutuunga mkono,” alisema Seif.

Alipoulizwa kuhusu mkutano huo, Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Uhusiano wa Umma, Salim Abdallah Bimani upande wa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alisema chama kipo imara na hakuna mjumbe atakayejitokeza kushiriki mkutano unaoitishwa na upande wa Lipumba.

Alisema wanaoratibu mipango ya mkutano huo wanaonyesha dalili za kuishiwa kisiasa na kuwataka wana CUF kuwapuuza.
Na hamisi Fakhi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
CUF WAJIPANGA MKUTANO MKUU CUF WAJIPANGA MKUTANO MKUU Reviewed by By News Reporter on 5/30/2018 05:28:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.