Loading...

UWANJA WA NDEGE KUTOA NAFASI ZA AJIRA 400

Loading...
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa jengo jipya la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar (Terminal III), zaidi ya ajira 400 zitapatikana.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Dk Sira Ubwa Mamboya alisema hayo baada ya kutembelea uwanja huo na kuongeza kuwa kipaumbele cha ajira hizo kitakuwa ni vijana.

Alisema Serikali inakusudia kuwapa elimu vijana ili waendane na uhitaji wa huduma zitakazotolewa kiwanjani hapo.

Dk Sira alisema kukamilika kwa ukarabati huo kutatoa fursa kwa ndege kubwa kutua Zanzibar, jambo aliloeleza kuwa litasaidia kukuza utalii.

Mratibu wa jengo hilo, Yasser Decosta alisema watahakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati ili watoe huduma bora kwa abiria.

Alisema ujenzi huo unaohusisha sehemu ya kuegesha ndege, magari na maeneo ya bustani utagharimu Dola 128 milioni za Marekani na utakamilika Januari mwakani.
Na Paskali Joseph.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
UWANJA WA NDEGE KUTOA NAFASI ZA AJIRA 400 UWANJA WA NDEGE KUTOA NAFASI ZA AJIRA 400 Reviewed by By News Reporter on 5/30/2018 05:37:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.