Loading...

HAWA NDIO WATU WENYE USHAWISHI ZAIDI DUNIANI

Loading...
Kiongozi wa China Xi Jinping ndiye mtu mwenye ushawishi Zaidi duniani, kwa mujibu wa jarida la Forbes. Amechukua nafasi hiyo baada ya bunge China kumpa mamlaka zaidi na kuondoa kikomo muhula wa rais.

Jingping amechukua nafasi hiyo kutoka kwa Rais Vladimir Putin wa Urusi ambaye anashika nafasi ya pili kwa kuwa alichaguliwa kuongoza kwa muhula wa nne kwa karibu 77% ya kura.

Rais wa Marekani Donald Trump ameshuka hadi nafasi ya tatu mwaka huu. Rais huyo amekuwa na kashfa kadhaa tangu mwanzo wa muhula wale 2016.

Wanne ni mwanamke mwenye ushawishi zaidi duniani, Angela Merkel. Kansela huyo wa Ujerumani alishinda kuongoza muhula wa nne mwaka 2017.

Mkuu wa Amazon Jeff Bezos ni wa tano na ndiye pia mtu tajiri zaidi duniani. Anamiliki 16% ya hisa za Amazon.

Papa Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, ni wa sita. Ni kiongozi wa kidini wa watu karibu 1.2 bilioni.

Bill Gates ni wa saba. Mwanzilishi huyo wa Microsoft aliuza sehemu kubwa ya hisa zake lakini bado yuko kwenye bodi.

Mwanamfalme wa kwanza mstari wa warithi Saudi Arabia Mohammed bin Salman Al Saud ni wa nne. Mwaka 2017 aliongoza kampeni ya kupambana na rushwa na kuwakamata watu wengi mashuhuri Saudia.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ni wa tisa. Ndiye kiongozi wa pili kufuatwa zaidi kwenye twitter, anawafuasi 43M. Aliyempita ni Trump pekee.

Larry Page ndiye wa kumi. Ni bilionea mwanzalishi mwenza wa Google, iliyoanzishwa kama mradi wa wanafunzi mwaka 1998.
Na Neema Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
HAWA NDIO WATU WENYE USHAWISHI ZAIDI DUNIANI HAWA NDIO WATU WENYE USHAWISHI ZAIDI DUNIANI Reviewed by By News Reporter on 5/12/2018 11:26:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.