Loading...

JANET JACKSON ATUMBUIZA AKIVALIA UREMBO WA KIMAASAI, TUZO ZA BILLBOARD

Loading...
Usiku wa Jumapili, Mwimbaji, muigizaji na mtumbuizaji kutoka nchini Marekani, Janet Jackson alitunukiwa tuzo ya Iconic katika tuzo za muziki za Billboard huko Las Vegas.

Hata hivyo, kilichostajaabisha mashabiki wengi waliotazama tuzo hizo hasa kutokea barani Afrika ni vile alivyoonekana tofauti kwa kuvaa mavazi yenye urembo wa kimaasai shingoni mwake.

Janet alipanda jukwaani akiwa amevalia shati lenye darizi za dhahabu na buti alizomechisha shati hilo pia zilikuwa za rangi ya dhahabu.

Kabla ya kupokea tuzo hiyo, mwana mama Janet alinyamazisha ukumbi mzima kwa shoo ya kipekee aliyoifanya jukwaa hapo.

Ilikuwa ni siku ya kipekee na ya heshima kwa mwanamuziki mkongwe, mwenye miaka 52 ambaye anaidadi kadhaa ya nyimbo zilizotamba kwa milongo kadhaa.
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
JANET JACKSON ATUMBUIZA AKIVALIA UREMBO WA KIMAASAI, TUZO ZA BILLBOARD JANET JACKSON ATUMBUIZA AKIVALIA UREMBO WA KIMAASAI, TUZO ZA BILLBOARD Reviewed by By News Reporter on 5/25/2018 10:58:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.