Loading...
Msaidizi Mkuu wa chuo kikuu cha Nairobi Peter Mbith akizungumza na waandishi wa habari amefahamisha kuwa kwa mara ya kwanza satellite iliyotengenezwa na wahandisi wa chuo hicho wakishirikiana na shirika la JAXA la Japan itarushwa angani kutokea Japan.
Zoezi hilo la kurushwa kwa satellite hiyo litaoneshwa moja kwa moja kupitia rundinga ya taifa.
Hatua hiyo ikifanikiwa basi Kenya itakuwa imeingia katika orodha ya mmataifa ya bara la Afrika yaliyowahi kurusha satellite angani.
Mataifa ya bara la Afrika ambayo yalikwisharusha sattelite ni Afrika Kusini,Nigeria,Algeria na Misri.
KENYA KURUSHA SATELLITE YAKE YA KWANZA
Reviewed by By News Reporter
on
5/09/2018 03:30:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: