Loading...
Jaji wa jjiji la New York, Marekani mwishowe ameagiza kijana wa miaka 30, asiye na kazi ahame kutoka katika nyumba ya wazazi wake baada ya wazazi hao kujaribu kumfukuza mtoto huyo kwa miezi kadhaa na bila mafanikio yoyote.
Siku ya Jumanne wakisikiliza maamuzi ya mahakama walipofika kusikiliza hukumu ya kesi hiyo, Mark na Christina Rotondo wa Camillus, New York pamoja na mtoto wa kiume Michael, ilisikika ikisemwa kijana wao huyo wa pekee asiyeajiriwa halipi kodi, na kutoa msaada wa namna yoyote hapo nyumbani kwao.
Jaji Donald Greenwood ambaye alikuwa akiendesha kesi hiyo alisikia wazaze wake wakisema walijitahidi kumfukuza kwa miezi kadhaa sasa lakini ilishindikana, mpaka walipokwenda kwake kuomba msaada ndio ikawezekana.
Kwa mujibu wa mtandao wa Mail Online, Michael alijitetea na kusema sheria inamruhusu kukaa kwa kipindi cha miezi sita kabla hajaondoka nyumbani hapo lakini jaji huyu alipinga madai kwamba ni kinyume na utaratibu kwa kuwa alivunja maagizo ya mwanzo ya wazazi wake. Na Michael alimwambia jaji kuwa hakutendewa haki na atakata rufaa kwa kuwa jaji hajaamua kesi ipasavyo huku akiondoka mahakamani hapo bila ya kuongea na wazazi wake vizuri.
Baadae jaji Donald aliwaagiza wazazi wa Michael kuja Nakala ya amri ya kufukuzwa kwa Michael ili aweze kuisaini. Lakini haijaamuliwa ni muda gani atapewa ili kuondoka nyumbani hapo.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

KIJANA WA MIAKA 30 AFIKISHWA MAHAKAMANI NA WAZAZI WAKE KWA KUGOMA KUONDOKA KWAO
Reviewed by By News Reporter
on
5/23/2018 02:00:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: