Loading...

MAHAKAMA NCHINI MISRI YAAMURU KUFUNGWA KWA YOUTUBE

Loading...
Mahakama kuu imeamuru kufungwa kwa You Tube nchini Misri.

Kwa mujibu wa habari,You Tube itafungwa kwa muda wa mwezi mmoja nchini humo.

Hii ni baada ya wakili mmoja wa Misri  kuifungulia kesi You Tube mwaka 2012 kwa madai ya kurusha video zinazomdhalilisha Mtume Muhammad.

Februari 2013,mahakama iliamrisha kufungwa kwa muda kwa You Tube nchini humo.

Hata hivyo kesi hiyo iliendelea kusikilizwa baada ya kukata rufaa.

Wizara ya mawasiliano nchini humo haijazungumza lolote  kuhusu suala hilo.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MAHAKAMA NCHINI MISRI YAAMURU KUFUNGWA KWA YOUTUBE MAHAKAMA NCHINI MISRI YAAMURU KUFUNGWA KWA YOUTUBE Reviewed by By News Reporter on 5/27/2018 11:43:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.