Loading...
Katika kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kimeandaa mdahalo wa wanataaluma huku Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki akialikuwa kuwa mgeni rasmi.
Mada kuu katika mdahalo huo utakaofanyika Mei 18, 2018 na kuwahusisha wanataaluma kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini pamoja na viongozi wastaafu na walioko madarakani ni hali ya elimu katika Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumamosi Mei 12, 2018 mjini Dodoma, Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Egid Mubofu amesema mhadhara huo ni mwanzo wa mihadhara itakayokuwa inafanyika kila mwaka chuoni hapo kwa ajili ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere.
Amesema chuo hicho kitakuwa kinafanya mihadhara mbalimbali ya kitaaluma.
Amesema Mbeki ataambatana na mkuu wa chuo hicho, Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ambaye siku za hivi karibuni alipendekeza kufanyika kwa mdahalo wa kitaifa kujadili sekta ya elimu nchini.
Na Fatma Pembe.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

MKAPA, MBEKI KUTIKISA MDAHALO WA ELIMU UDOM
Reviewed by By News Reporter
on
5/13/2018 09:20:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: