Loading...
Mkenya mmoja mbunifu amewashangaza wengi baada ya kubuni mbinu ya hadha ya msongamano na foleni ya magari huko jijini Nairobi.
Morris Mbetsa ametengeneza gari la kwanza nchini lenye uwezo wa kupaa angani.
Mbetsa aliweka wazi kuwa mradi wake unakusudia kutumika kama teksi jijini Nairobi.
"Ni gari ndogo na linalopaa kwa urefu mdogo, juu kidogo ya msongamano wa kawaida na yenye nafasi finyu ya kusababisha matatizo." Alisema Mbetsa Jumatano, Mei 2 akifanyiwa mahojiano na mtandao mmoja huko Kenya.
Katika picha zilizopatikana katika gereji hiyo alionekana mfanyakazi mmoja akiendelea kutengeneza gari hilo la jaribio ambalo lina umbo la helikopta.
Mbetsa alieleza kuwa mradi huo utakaomgharimu Ksh 8 milioni sawa na pesa za Kitanzania zaidi ya Milioni 180, unaweza kuimarisha sekta ya uchukuzi.
"Ninaamini kuwa nikipata pesa zaidi kwa mradi huu, nitabuni mambo mengi ikiwemo mfumo wa kudhibiti hewa na sehemu maalum za kutua na kupaa kwa gari hiyo." Mbetsa alisema.
Gari linalopaa na lililotengenezwa kutoka kwa nyenzo za kaboni halitumii mafuta kama magari mengine.
Inatumia betri maalum ambayo inaongezwa nguvu kwa kutumia umeme kwa saa kadhaa ili iweze kupaa kwa dakika 20 ikiwa uzito unaostahili utadumishwa.
Gari hilo lenye propela na magurudumu ni ndogo na haiwezi kuwatatiza wakazi wengine wa jiji.
“Kwangu, ubunifu ni kama Mpesa ambayo iliiweka Kenya kwenye ramani ya dunia. Hakuna aliyeamini kuwa ubunifu wa aina hiyo uliweza kutokea Afrika.”
Morris alieleza. Morris alianza kubuni vitu tofauti mwaka wa 2009, akibuni mfumo unaoweza kutumia simu kufunga gari na kulizuia kuibiwa alipokuwa na miaka 19.
Kwenye mradi wake wa hivi punde, analenga kuzindua gari lake la kwanza la kupaa angani.
Na Paskali Joseph.
Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za teknolojia punde zinapojiri.

MKENYA ABUNI GARI INAYOPAA ANGANI
Reviewed by By News Reporter
on
5/03/2018 03:31:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: