Loading...

TAHADHARI MVUA KUBWA YA SIKU TANO

Loading...
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa juu ya wastani kwa siku tano mfululizo zinazoweza kusababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na TMA, mvua hizo zimeanza juzi Mei Mosi na zitaendelea mpaka Mei tano mwaka huu na zinatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga pamoja na visiwa vya Pemba na Unguja.

Mikoa mingine itakayoathirika na mvua hizo ni Mara, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Katavi, Kigoma, Arusha, Kilimanjaro na Manyara.

TMA imesema kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni pamoja na mafuriko katika baadhi ya maeneo na kuathiri jamii, adha ya usafiri kwa barabara kubwa kutopitika.

Kwa mujibu wa TMA athari za mvua hizo ni kujaa kwa maji au yanayopita kwa kasi na kuhamishwa kwa watu kutoka maeneo yaliyoathiriwa.

Angalizo lingine ni upepo mkali na mawimbi makubwa kwa maeneo ya ukanda wa Pwani inayojumuisha mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara pamoja na Visiwa vya Pemba na Unguja.
Na Geofrey Okechi.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za kitaifa punde zinapojiri.
TAHADHARI MVUA KUBWA YA SIKU TANO TAHADHARI MVUA KUBWA YA SIKU TANO Reviewed by By News Reporter on 5/03/2018 03:05:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.