Loading...

MLIMBWENDE 'TAMARYN' ALIYESHINDA TUZO YA UREMBO AFRIKA KUSINI 2018

Loading...
Ilikuwa jioni ya ladha na furaha baada ya mrembo Tamaryn Green mwenye miaka 23, pale alipovishwa taji la Ushindi wa Urembo wa Afrika ya Kusini 2018.

Tamaryn aliwashinda warembo 11 katika kinyang'anyiro hicho, pia ataenda kuiwakilisha nchi ya Afrika Kusini katika Mashindano ya kuwania Taji la Mrembo wa Dunia.

Mlimbwende Tamaryn alifanywa kuwa juu baada ya kumshindwa kwa pointi nyingi mrembo mwenzake mwenye miaka 26, muhitimu katika Chuo Kikuu cha Cape Town aliyefahamika kwa jina Thulisa Keyi, ambaye alikuwa wa pili.

Tamaryn ni mwanafunzi katika fani ya udaktari kutokea Western Cape. Alijinyakulia pointi nyingi baada ya kuwaambia majaji kwamba atatumia taaluma yake kuwatibu watu.
Na Neema Bushubo.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MLIMBWENDE 'TAMARYN' ALIYESHINDA TUZO YA UREMBO AFRIKA KUSINI 2018 MLIMBWENDE 'TAMARYN' ALIYESHINDA TUZO YA UREMBO AFRIKA KUSINI 2018 Reviewed by By News Reporter on 5/29/2018 01:39:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.