Loading...
Kulingana na imani, sadaka huwa ni matoleo ya mapato ya kazi yako, ikitegemea kazi unayoifanya.
Katika mila za Kiafrika, mtu anastahili kupeleka madhabahuni fungu la kumi na mazao ya kwanza ya shamba kama zaka, ila kwa jamaa huyu aliyeiga mwelekeo huo mambo kwake yalikuwa tofauti.
Jamaa mmoja kutoka Meru alifika kanisani akiwa amebeba gunia la miraa (mirungi) kama sadaka ila waumini na hata kiongozi wa kanisa wakamgeukia na kumfurusha kama mbwa.
Kwa mujibu wa gazeti la Taifa Leo nchini Kenya, pasta wa kanisa hilo alikuwa amewakubalia waumini kutoa mavuno yao kama sadaka ambayo yangeuzwa baadaye na kubadilishwa kuwa pesa.
Kama kawaida, watu walikuja na mavuno mbalimbali ya shambani lakini jamaa huyo aliamua kuleta mavuno ya shamba lake, mirungi.
Na Hamisi Fakhi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

MUUMINI ATIMULIWA KANISANI KWA KUPEREKA GUNIA LA MIRUNGI KAMA SADAKA
Reviewed by By News Reporter
on
5/11/2018 04:41:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: