Loading...

MWANAMKE WA MIAKA 24 AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSHIRIKI NGONO NA MWANAFUNZI WA DARASA LA 7

Loading...
Mwanamke wa miaka 24 kutoka Kisumu, Kenya alipatikana na makosa ya kushiriki ngono na mtoto wa miaka 14 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba.

Bado hajahukumiwa kifungo jela kwa sababu ya kosa hilo baada ya Jaji Joan Wambilyanga, aliyetakiwa kutoa hukumu hiyo Jumatano, Mei 9, alisema hayupo tayari kuhitimisha na kutoa hukumu.

Aliaja siku nyingine ya kutoa hukumu yake kuwa ni Mei 23. Kulingana na ripoti ya Daily Nation iliyotaarifu kuwa, Wambilyanga alipatikana kuwa na makosa ya kushiriki ngono na mwanafunzi huyo wa darasa la saba, ambaye walikuwa wakiishi pamoja kama mke na mume kwa karibu miezi minne.

Wandera aliiambia mahakama kuwa alianza uhusiano na mwanafunzi huyo walipokutana ndani ya baa moja. 

Kwa kujitetea, alisema hakujua kijana huyo alikuwa wa umri mdogo kwa sababu alificha umri wake kwa sababu ya nywele kubwa(rasta) aliyokuwa akifuga, na zilizomfanya kuonekana kama mtu mkubwa. 

Alimdanganya kuwa alikuwa mwendeshaji pikipiki ambaye alikuwa akiendelea vizuri maishani baada ya kufukuzwa nyumbani na wazazi wake waliomshutumu kwa kusema alikuwa mzembe. 

Kutokana na stori yake ya kusikitisha, aliingia mtegoni, asijue alikuwa mtoto mdogo, wa miaka 14 na mwanafunzi.
Na Peter Godwin.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MWANAMKE WA MIAKA 24 AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSHIRIKI NGONO NA MWANAFUNZI WA DARASA LA 7 MWANAMKE WA MIAKA 24 AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSHIRIKI NGONO NA MWANAFUNZI WA DARASA LA 7 Reviewed by By News Reporter on 5/10/2018 11:50:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.