Loading...
Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi Maarufu ‘SUGU’ leo Mei 10, 2018 ametoka gerezani alikokuwa akitumikia kifungo cha miezi 5 jela ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kukamilisha adhabu hiyo.
Sugu ameachiwa kwa msamaha wa Rais Magufuli alioutoa tarehe 26 Aprili, 2018 katika maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanzania.
Nampongeza Rais Magufuli kwa kuonesha ukomavu wa kisiasa maana kwa kosa la kumtusi alilolifanya Sugu, mtu mwingine angetaka kumkomoa kwa kumuengua na msamaha huo. Na hili limefanyika mahali pengi.
Rais Magufuli hajajali mambo ya kisiasa na maumivu ya matusi aliyotukanwa na Sugu wakati wa uchaguzi mdogo wa udiwani huko Mbeya. Hili ni jambo muhimu na la kupongezwa sana, inawezekana wengine wasione lakini ukweli ni kwamba inaleta faraja kwamba tuna Rais ambaye ana ukomavu wa kisiasa.
Naamini Sugu mwenyewe na wanasiasa wengine watakuwa wamejifunza kwa hili, na watatambua umuhimu wa kufanya siasa za kistaarabu badala ya kupotomosheana matusi ambayo hayalijengi Taifa letu na yanaharibu sifa na heshima ya Tanzania.
Na Godwin Mbaningo.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

HABARI ZA HIVI PUNDE: SUGU ATOKA JELA LEO KWA MSAMAHA WA RAIS MAGUFULI
Reviewed by By News Reporter
on
5/10/2018 10:22:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: