Loading...
CHUO Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) kupitia kitengo cha udhibiti wa viumbe hai waharabifu kimefanya utafiti kutumia mkojo wa paka kuzuia panya waharibifu wa mazao kwa wakulima.
Hayo yalisemwa jana na mtafiti na mtoa ushauri kitengo cha uthibiti wa viumbe hai waharibifu wa huo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Profesa Mulungu Moth alipozungumza na gazeti moja hapa nchini.
Profesa Moth alisema kuwa baada ya wakulima kupata athari kubwa ya mazao yao kuliwa yakiwa shambani na viumbe hai waharibifu, SUA kufanya utafiti mbalimbali ukiwemo wa kutumia mkojo wa paka kuzuia panya wasiingie mashambani kula mazao.
Alisema utafiti uliofanyika mkoani Iringa eneo la Isimani kuhusu uharibifu wa panya mwaka 2013 - 2015, ulibaini kuna aina 200 za panya na kati yao aina 31 wanaitwa panya shamba na ndio waaribifu mazao.
Profesa Moth alisema panya shamba hao wana uwezo wa kuzaliana kwa wingi kipindi cha mvua wakulima wakiwa wanapanda mazao yao ikilinganishwa na wakati wa ukame ama jua kali.
Alitoa mfano maeneo ambayo 'Panya Shamba' wameweza kuharibu mazao kuwa ni pamoja na Wilaya ya Kilombero na Morogoro na maeneo mengi nchini.
"Panya licha ya kudhibitiwa kwa kuweka mitego, sumu, ndoo, kufuga paka, kuweka bundi na nyoka bado changamoto hiyo haijaweza kuleta ufanisi mkubwa.
"Kutokana na changamoto hiyo SUA tumezidi kufanya utafiti na kubaini kuwa mkojo wa paka unaweza kutengenezwa maabara na harufu yake inaweza kufukuza panya waharibifu.
Hata hivyo, alisema endapo dawa yenye mchanganyiko wa mkojo wa paka itatengenezwa kiwandani, itasaidia usalama wa chakula na kuondoa tishio kwa wananchi.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

UTAFITI: MKOJO WA PAKA KUZUIA PANYA WAHARIBIFU
Reviewed by By News Reporter
on
5/10/2018 10:15:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: