Loading...
Wanandoa mjini Mombasa wameitaka mahakama kuvunja ndoa yao ya miaka 22 kwa sababu ya uzinzi na kunyimana haki za ndoa.
Mke katika ndoa hiyo ya wawili aliamua kufika mahakamani kuvunja ndoa yao bila kurudi nyuma na uamuzi wake.
Kulingana na mtandao wa Daily Nation, mwanamke huyo kupitia wakili wake alimshutumu mumewe kwa kutelekeza familia yake kwa kipindi cha muda wa miaka 5.
Wawili hao walioana eneo la jomvu Kuu Mombasa mwaka 1996 na walibahatika kupata watoto wawili hadi sasa ni watu wazima.
Mama huyo alieleza mahakama ndoa yake ilikuwa salama mpaka 2007 mpaka alipogundua kuwa mumewe ana nyumba ndogo.
Alidai mwanaume huyo alipata mtoto wa nje ya ndoa katika uhusiano huo na ndicho chanzo au kiini kikubwa cha migogoro katika ndoa yao.
"Kuanzia 2013 mume wangu alininyima unyumba mpaka sasa kwani alihama chumba chetu cha kulala na kuanza kulala chumba kingine. Hali ilinifanya kuhisi sina thamani," aliiambia mahakama.
Alieleza mahakama kuwa juhudi za kuokoa ndoa yake zimegonga mwamba hata baada ya kukutana na wazazi wao mara kadhaa.
Na Catherine Kisese.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

MWANAMKE ADAI 'TALAKA' BAADA YA KUNYIMWA UNYUMBA KWA MIAKA 5
Reviewed by By News Reporter
on
5/05/2018 10:57:00 AM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
5/05/2018 10:57:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: