Loading...

JAMAA AMSHAMBULIA MGANGA KWA KUMPA NDUMBA FEKI

Loading...
Kilitokea kioja katika eneo la Kiembeni, Mombasa huku jamaa kumfurusha mganga aliyekuja kumdai malipo baada ya kumhudumia jamaa huyo.

Kwa mujibu wa gazeti moja huko Kenya, jamaa huyo alikuwa mteja wa mganga huyo kwa muda mrefu ila hakuwahi kufanikiwa kutokana na Ndumba za mganga wake.

"Baada ya jamaa kupewa dawa kwa mara ya kwanza, hakufanikiwa kupata kazi na kadri alivyozidi kumtembelea mganga huyo ndivyo mambo yalizidi kumuendea mrama.," Mdukuzi alinukulia na gazeti hilo.

Siku ya kisa hicho, mganga alifunga safari hadi kwa mteja wake kudai malipo yake.
Alipofika hakuamini kilichomsibu.

Mteja wake aliinuka kwa hasira tayari kumvamia punde tu alipomuona.

"Unaenda wapi mganga feki kama wewe? Nani alikupa mwaliko wa kunitembelea? Sitaki kukuona hapa kwangu. Unanidai nini na hizi hirizi zako zimeshindwa kufanya kazi. Ndumba zako ni feki na tangu nilipoanza kuzitumia sijawahi kufanikiwa hata kidogo. Kama umekuja kudai malipo, pole sana maana sikupi hata senti moja. Ondoka hapa mara moja," jamaa alimfokea mganga.

Jamaa huyo baada ya kuona kuwa mambo ni magumu, alianza kutisha jamaa huyo.

"Ukijaribu kucheza na mimi utakiona cha mtema kuni. Nakupa siku saba uniletee pesa zangu na ukikataa yatakayokupata usije kunitafuta." Mganga huyo alimtishia mteja wake.

Jamaa alisimamia msimamo wake bila kuyumba alichosema. "Hata ukitoa vitisho kiasi gani sina shaka maana najua wewe ni mganga feki. Sitaki blah blah blah zako, bure kabisa wewe."

Mganga huyo alilazimika kuondoka huku jamaa huyo akimshambulia kwa maneno kuwa hatothubutu kuomba msaada wa mganga yeyote tena.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
JAMAA AMSHAMBULIA MGANGA KWA KUMPA NDUMBA FEKI JAMAA AMSHAMBULIA MGANGA KWA KUMPA NDUMBA FEKI Reviewed by By News Reporter on 5/05/2018 11:36:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.