Loading...

MWANASAYANSI ALIYEOMBA KUJITOA UHAI, AFIKIA TAMATI

Goodall mwenye miaka 104 alizaliwa jijini London Aprili mwaka 1914 ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kuanza Vita ya Kwanza ya Dunia, na alikuwa mtaalam wa sayansi ya viumbe na maisha ya wanyama.  Alisafiri kutoka magharibi mwa Australia hadi Basel, Uswiss, kwa ajili ya kujitoa uhai kwa hiari, ingawa alisema anachukizwa na kitendo hicho.

Goodall amehitimisha safari yake ya mwisho akiwa amezungukwa na familia yake ambapo alishika bomba la sindano yenye sumu aina ya Sodium pentobarbital na kusukuma kwenye mwili wake, ambapo iliingia kwenye mishipa ya damu na sumu  ikaenea mwilini na kupoteza uhai wake.
Loading...
uSd34snIwFE4ZXJ99j0OdgV3WnL6XhXyuDqf46mdVAcvjgFYtrn0wK-n_B-TgU2-JKaADXXSCurSoyZDtAAz25svf71uHT3/s1600/akizungukwa+na+familia+yake.jpg"> Chakula chake cha mwisho kilikuwa ni samaki, chipsi na keki  huku akisikiliza wimbo wa Beethoven, Ninth Symphony.

Wakati wa pumzi yake ya mwisho, Goodall aligeuza kiti na kuruhusiwa kujichoma sindano hiyo ambapo kwa nchi kama Canada, Uholanzi, Luxembourg, Uswiss na sehemu nyingine za Marekani, sheria inaruhusu mtu kuamua kujiua kwa sababu maalum.

Wasamaria wema walimchangia Dola 20,000  za Marekani ambazo ni sawa ni zaidi ya Tsh. 45 milioni ili kumsaidia kutimiza azma yake hiyo. Hata hivyo, kabla ya kufikia uamuzi huo, alisema kwamba kinachomfanya aharakishe kufa ni kutokana na kupungua kwa uhuru unaosababishwa na  umri.

Mwili wake utachomwa moto nchini Uswiss na kisha majivu kupelekwa Australia.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MWANASAYANSI ALIYEOMBA KUJITOA UHAI, AFIKIA TAMATI MWANASAYANSI ALIYEOMBA KUJITOA UHAI, AFIKIA TAMATI Reviewed by By News Reporter on 5/11/2018 05:59:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.