Loading...
Inakadiriwa kuwa asilimia 60 ya wananchi wa Tanzania ni vijana wenye umri zaidi ya miaka 18.
Ili kuonyesha kuna ushindani mkali katika soko la ajira, kila mwaka kuna vijana takriban 800,000 wanaomaliza shule za msingi, sekondari na vyuo na hatimaye kuanza kusaka ajira.
Ushindani huo ndiyo unaotoa changamoto kubwa kwa vijana kusaka ajira hizo.
Achilia mbali mifumo yetu ya elimu kama inamwezesha kijana kujiajiri au kuwa na ujuzi wa kiasi gani, lakini ni jukumu la kila kijana kuhakikisha kuwa anapata fursa ya ajira.
Kuna njia mbalimbali za kumwezesha kijana kuajiriwa au kujiajiri mwenyewe. Njia hizo hazijalishi elimu aliyonayo kijana kwa sababu mtu anaweza kuwa na elimu ya chuo kikuu, lakini akakosa ajira huku mwenye elimu ya kidato cha nne akiajiriwa.
Kwanza ni lazima kijana ajue anapenda kazi gani. Wapo vijana wana vipaji au wito na kazi fulani. Kwa mfano, mtu ana kipaji cha muziki, kuchora picha au hata kuongea au kuchekesha.
Vipaji hivi vinaweza kuwa chachu ya mtu kuajiajiri na kufanikiwa.
Wazazi nao wana mchango mkubwa wa kuwaelekeza watoto kwenye vipaji vyao wanapovitambua.
Kwa hiyo, kijana anayejitambua anapaswa kuvifanyia mazoezi vipaji vyake ili abobee kwenye fani husika.
Kwa upande mwingine, uzoefu unaonyesha kuwa, vijana wengi waliojiajiri ni wale waliopata elimu ya chini wakajikita kwenye ujuzi fulani kwa muda mrefu kisha wakabobea na kujikuta wakijiajiri.
Kwa hiyo utaona ili kijana ajiajiri na adumu kwenye hiyo ajira, ni lazima apate uzoefu kwenye eneo fulani.
Kwa mfano, wapo vijana wanaomiliki karakana za ufundi seremala, ufundi makenika, uchomeleaji wa vitu kama vile samani na vinginevyo.
Vijana kama hawa hudumu kwenye ajira zao kwa sababu wameanzia chini hatua kwa hatua na wamejikuta wakiwa na nidhamu ya kazi hadi wakafanikiwa kimaisha. Kijana wa aina hii hawezi kutetereka kiuchumi.
Vijana hao ni tofauti na vijana ambao hupewa mitaji na wazazi au ndugu zao na kuainisha biashara au miradi bila kuwa na uzoefu, matokeo yake hufilisika kirahisi.
Kwa wale wanaotafuta kuajiriwa, nao wanapaswa kujitambua mapema kazi wanazotafuta. Kwa mfano, mtu umesomea uhandisi wa majengo na ukiwa masomoni umewahi kufanya mazoezi ya kupata ujuzi. Hiyo ndiyo nafasi ya kutokea.
Unachotakiwa ni kujenga mtandao wa mawasiliano na kampuni za ujenzi na wadau wa fani yako.
Vilevile jenga uaminifu kwa watu na kampuni husika, ili hata ukimaliza shule iwe rahisi kuitwa kwenye ajira.
Njia ya pili ni kuonyesha ujuzi wako kwa mwajiri unayetaka akuajiri.
Waajiri wengi wanataka mtu mwenye utayari, wanataka waone kazi inafanyika, vyeti ni jambo la pili.
Kama wewe unapenda uandishi wa habari, andika habari na hakikisha zinatoka au tangaza kama ni redioni au kwenye runinga watu wakuone.
Kuna msemo wa Wahenga usemao; Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza.
Vijana wengi wanamaliza vyuo vikuu, wanakalia kuzunguka na vyeti vya shule kwa muda mrefu bila ajira. Yote ni kwa sababu hawakuwa na matayarisho wakiwa shule.
Mambo ya msingi ya kuzingatia unapojiajiri au kuajiriwa, kwanza ni kubobea kwenye fani fulani kama vile ufundi seremala, ufundi uashi, ufundi makenika, upishi, udereva na kazi nyinginezo za kitaaluma.
Jambo la pili ni kuwa na nidhamu ya kazi. Jali muda wa kufika kazini na ufanye kazi kwa bidii hata kama kwa wakati huo haina kipato kikubwa.
Heshimu wafanyakazi wenzako na uwe na uhusiano mzuri nao pia ni lazima uwe na na nidhamu ya matumizi ya pesa kwa kujiwekea akiba.
Jambo la tatu ni kuwa na malengo. Kwa kazi yoyote unayofanya ni lazima ujue kuna majukumu makubwa mbele yako kama vile kuwa na familia, kusaidia ndugu na jamaa na kujiendeleza.
Ni lazima kujiwekea malengo makubwa yatakayoongeza kipato cha kukabiliana na majukumu ulionayo.
Tunalilia ajira na ni haki yetu kuwa nazo, wafanyabiashara wadogo nao wanalilia mitaji na mikopo.
Hata hivyo, hivi vyote havitokuwa na tija kama kwanza hatutobadili mifumo ya maisha na mitazamo.
Tukiwa wavivu wingi wa viwanda tunavyoahidiwa kujengewa hautafaa kitu maana mikopo na mitaji itaishia kwenye starehe.
Tukitaka mabadiliko ya kimaisha, vijana kwa mfano wabadili fikra kuwa maisha yanaweza kupatikana kwa urahisi kwa kujikita katika kulima bustani za mboga au kujihusisha na ufugaji wa aina mbalimbali ya mifugo.
Vijana tusipojipinda wenyewe kwa kubadili fikra kuhusu kazi na maisha kwa jumla tusahau maendeleo maana hayaji kirahisi isipokuwa ni kwa kutoka jasho jingi, kuwa wabunifu na kutumia vyema fursa zilizopo. Ni vyema tupambane sasa.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

NI RAHISI KWA KIJANA KUJIAJIRI AU KUAJIRIWA
Reviewed by By News Reporter
on
5/09/2018 01:17:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: