Loading...

'SINA MPANGO WA KUZAA KWA SASA' - LULU DIVA

Loading...
Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na wimbo wake wa ‘Huba’ Lulu Diva amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kuzaa mtoto kwa hivi sasa labda baada ya miaka mitano.

Kama utakumbuka siku mwezi uliopita wakati Lulu Diva anasheherekea siku yake ya kuzaliwa (birthday) CEO wa WCB Diamond Platnumz alianika wazi uhusiano wake na Rich Mavoko na kumtaka Lulu Diva Azae naye mtoto.

Kwa kipindi kirefu Kumekuwa na tetesi za Lulu Diva kuwa na Mahusiano ya kimapenzi na Rich Mavoko ingawa wawili hao wamekuwa wakikataa na hata kuficha lakini wamebambwa pamoja mara kadhaa.

Kwenye mahojiano ambayo Lulu Diva alifanya na Sam Misago Tv, ameweka wazi licha ya kuwa Diamond alimtaka azae mtoto hivi karibuni na yeye akakubali hjamaanisha atazaa siku za hivi karibuni kwani hana mpango wa kuzaa mpaka miaka mitano ipite.

"Mbona mimi kila siku ninasemaga siwezi kupata mtoto sahivi labda miaka mitano sita huko na kuendelea sio sasa hivi kabisaaa”.

Lakini pia Lulu Diva aliendelea kukataa kuongelea Mahusiano Yake na Rich mavoko huku akidai hayo ni maisha yake binafsi na asingependa kuyaani.
Na Neema Bushubo.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
'SINA MPANGO WA KUZAA KWA SASA' - LULU DIVA 'SINA MPANGO WA KUZAA KWA SASA' - LULU DIVA Reviewed by By News Reporter on 5/10/2018 08:00:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.