Loading...

WAREMBO WAWILI WAZICHAPA LIVE KUMGOMBEA BABA WA DIAMOND

Warembo wawili ambao walifahamika kwa majina ya Ashura na Zubeda, wamedaiwa kuzichapa kavukavu chanzo kikitajwa kuwa ni kumgombea baba wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma.

Tukio hilo lililokusanya watu lilitokea hivi karibuni katika baa moja maarufu kwa jina la Suma iliyopo maeneo ya Magomeni-Kagera jijini Dar ambayo baba wa msanii huyo anadaiwa kuwa anakwenda mara kwa mara kupata ‘kinywaji’.

Mtoa ubuyu wetu aliyelipigia simu Amani alisema kuwa, warembo hao walitangulia
Loading...
ufika katika baa hiyo na kupiga stori pamoja huku wakipata kilevi lakini baadaye alipotokea baba Diamond na kujumuika nao, kila mmoja alianza kujitapa kuwa ni wake. “Yani walianza kubishana. Ghafla wakaanza kushikana na ndipo watu walipowawahi na kuwaamua. Baba Diamond kukwepa soo akaamua kutoweka eneo hilo,” kilidai chanzo chetu.

Baada ya kuunasa ubuyu huo, Amani lilimvutia waya baba Diamond ambaye alishtuka kusikia habari zimetua gazetini na kusema: “Ni kweli lakini please naomba upotezee maana wale wote sio watu wangu wewe si unajua mimi nina mke wangu, mambo ya kilabuni hayo babu.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WAREMBO WAWILI WAZICHAPA LIVE KUMGOMBEA BABA WA DIAMOND WAREMBO WAWILI WAZICHAPA LIVE KUMGOMBEA BABA WA DIAMOND Reviewed by By News Reporter on 5/11/2018 07:00:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.