Loading...

WATU 180 WAMEFARIKI KUFUATIA MVUA KALI ZILIZONYESHA NCHINI RWANDA

Loading...
Watu wasiopungua 180 wameripotiwa kufariki kufuatia mvua kali zilizonyesha nchini Rwanda katika kipindi cha miezi minne. Taarifa kuhusu maafa yaliosababishwa na mvua kali hizo nchini Rwanda imetolewa  Jumamosi na serikali  na kutoa tahadhari  kwa raia katika siku 10 zijazo.

Mvua hizo zilisababisha hasara kama alivyofahamisha waziri wa  mazingira Vicent Biruta Jumamosi na kutoa tahadhari kwa raia. Tahadhari hiyo imetolewa kwa raia waliopo katika eneo la Kaskazini, Magharibi na Kusini-Magharibi mwa Rwanda.

Mvua kali Afrika Mashariki zimeripotiwa kuongezeka, nchini Kenya watu  watu zaidi ya 100 pia wamefariki katika mvua zilizonyesha Aprili nchini humo, nchini Tanzania , mvua kali zilisababisha hasara kama ilivyofahamisha na shirika la msalaba mwekundu.

Mwishoni mwa Juma, mjini Ankana nchini Uturuki mvua kali ilisabisha mafuriko yaliopelekea watu 6 kujeruhiwa.
Na Joseph Luwambi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WATU 180 WAMEFARIKI KUFUATIA MVUA KALI ZILIZONYESHA NCHINI RWANDA WATU 180 WAMEFARIKI KUFUATIA MVUA KALI ZILIZONYESHA NCHINI RWANDA Reviewed by By News Reporter on 5/09/2018 11:36:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.