Loading...
Nchi
wanachama wa mkutano wa shirika la afya duniani wamepitisha azimio la
kutambua kuumwa na nyoka kuwa ni suala linalohitaji kupewa kipaumbele
katika kulishughulikia.
Maelfu ya watu hufa kila mwaka na wengine kuwa walemavu kutokana sumu inayotokana na shambulio la nyoka.
WHO inasema athari zinazotokana na kuumwa na nyoka zimeendelea kuwa moja kati ya magonjwa ya kitropiki ambayo hayatiliwi maanani.
Kufikiwa makubaliano hayo kwa nchi wanachama wa WHO , kuna nia ya kuhakikisha kuwa kunakuwa na mbinu za kuzuia, kutibu na kukabili mashambulizi ya nyoka.
Makundi ya mbalimbali ya wanaharakati wa masuala ya afya yamesifia azimio hilo na kusema kuwa hatua hiyo inafungua milango katika kupunguza vifo na ulemavu duniani kote.
Shirika la Afya duniani sasa lina jukumu la kuja na mpango wa pamoja kuimarisha programu za tiba, kuzuia na kurekebisha.
Hii itahusisha kutoa dawa za kupambana na sumu kwa bei rahisi, dawa ambazo ilikua gharama kupatikana kwenye nchi zilizo masikini hasa zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.
Na Fatma Pembe.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

WHO YATOA TAHADHARI KUHUSU WATU KUUMWA NA NYOKA
Reviewed by By News Reporter
on
5/26/2018 12:17:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: