Loading...

GIGY MONEY ADAI ETI DIAMOND NI BABA WA MWANAE

Loading...
Msanii wa Bongo Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amerudi tena Kwenye headlines huku safari hii akidai Baba wa mtoto wake MK staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Gigy Money alijifungua mwezi uliopita lakini tangu ajifungue aliweka wazi kuwa hamjui baba wa mtoto wake kwani kipindi anapata mimba alikuwa Anatembea na wanaume wawili ambao alisema ni Mo J na Stan.

Lakini sahivi Gigy ameibuka na jipya akidai Baba wa mtoto wake pia anaweza kuwa Diamond Platnumz ambaye siku za nyuma zilishawahi kusikika tetesi kuwa aliwahi kuchepuka naye.

Gigy Money amefunguka hayo Kwenye mahojiano na Dizzim Online ambapo aliulizwa nani ni Baba wa mtoto na alifunguka:

"Mo J sio Baba wa mtoto nilishasema Baba wa mtoto anaitwa Naseeb Juma Abdul au Diamond ambaye nanona bora yeye awe Baba kwa sababu ni Mlezi wa wana alafu na mimi mwenyewe Mlezi wa wana alafu kingine anapenda watoto alafu alishanichanaga Gigy ukizaa we niambie tu kwa wiki shilingi ngapi”.

Gigy Money amekuwa sana Kwenye headlines tangu ajifungue kwani ni wikiendi iliyopita inasemekana alipeana kichapo cha mwizi na mrembo Irene club.
Na Mohamedi Makame.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
GIGY MONEY ADAI ETI DIAMOND NI BABA WA MWANAE GIGY MONEY ADAI ETI DIAMOND NI BABA WA MWANAE Reviewed by By News Reporter on 6/13/2018 01:44:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.