Loading...

HARMONIZE AFUNGUKA BAADA YA KUMWAGANA NA SARAH

Loading...
Staa wa muziki kutoka WCB Harmonize amefunguka kwa mara ya kwanza tangu sakata litokee wikiendi iliyopita na kusababisha yeye na mpenzi wake Sarah kutofautiana.

Harmonize na Sarah walikamata headlines mwishoni mwa wiki hii baada ya wawili hao kurushiana maneno Kwenye mitandao ya kijamii na hata matusi yaliyopelekea kumwagana baadae.

Harmonize anafunguka kuhusu sakata hilo na kuweka wazi kilichokuwa kinatokea pale ni wivu wa kimapenzi ambao Sarah anao juu yake hasa pale alipomuona akiwa na wadau wa muziki wa kike.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Wasafi Tv, Harmonize anafunguka kuhusu sakata hilo lililotokea kati yake na Mpenzi wake Sarah:

"Unapoamua kuwa na mtu unatakiwa ujue huyo mtu ni wa aina gani, anafanya kazi gani, ukishajua hivyo unakuwa ni rahisi zaidi ku-deal naye.

"Nakutana na watangazaji, wasanii inatakiwa ni badilishane nao mawazo, sasa ukiwa unaendekeza kila saa masuala ya kimahusiano inakuwa unanirudisha nyuma kwa namna moja au nyingine."

Harmonize ameweka wazi kuwa sakata  hilo lilianza baada ya Sarah kujaribu kumpigia kwa muda mrefu na yeye kutokana na kuwa bize na kazi alishindwa kupokea simu na hivyo kusababisha kukosa maelewano.
Na Fatma Pembe.





Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
HARMONIZE AFUNGUKA BAADA YA KUMWAGANA NA SARAH HARMONIZE AFUNGUKA BAADA YA KUMWAGANA NA SARAH Reviewed by By News Reporter on 6/13/2018 01:25:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.