Loading...

FAIZA ATHIBITISHA KUMALIZA BIFU LAKE NA SUGU

Loading...
Muigizaji wa Bongo movie Faiza Ally na mzazi mwenzake ambaye ni  Mbunge wa Mbeya Mjini Mheshimiwa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ wameonekana kumaliza bifu lao.

Faiza na Sugu wameshawahi kurushiana maneno Kwenye mitandao ya kijamii mara kwa mara na hata kufikia hatua ya Faiza kumtukana matusi ya nguoni mzazi mwenzake.

Hali ilikuwa mbaya baina yao hadi kufikia hatua ya Sugu kutopewa nafasi ya kumuona binti yao anayeitwa Sasha.

Lakini hivi sasa inaelekea hali ni shwari kwani Faiza ameweka picha Mtandaoni zinazomuonyesha Sugu akiwa na binti yake ambaye ameenda kumtembelea mkoani Mbeya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza aliweka picha ya Baba na mtoto na kusindika na ujumbe mfupi ili kudhihirisha kuwa hivi sasa hana tatizo na mzazi mwenzake huyo.
Na Neema Bushubo.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
FAIZA ATHIBITISHA KUMALIZA BIFU LAKE NA SUGU FAIZA ATHIBITISHA KUMALIZA BIFU LAKE NA SUGU Reviewed by By News Reporter on 6/13/2018 01:15:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.