Loading...
Wanafunzi wawili na watumishi wawili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wataagwa kesho katika ukumbi wa Nkurumah, chuoni hapo.
Wanafunzi na watumishi hao wa UDSM, walifariki katika ajali iliyohusisha gari la kubebea wagonjwa (ambulance) na lori la mizigo eneo la Riverside, Ubungo.
Waliofariki wote walikuwa ndani ya gari la kubebea wagonjwa aina ya Toyota Land Cruser na lilikuwa likitokea zahanati ya hosteli za chuo hicho za Mabibo kuwapeleka kituo cha afya cha Kampasi.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Chuo hicho Profesa William Anangisye jana (Juni 12) ilieleza kuwa waliofariki katika ajali hiyo ni James Rutayuge (Dereva mwandamizi), Jonathan Rung’ando (Muuguzi msaidizi daraja la pili), Erasto Sango (Mwanafunzi wa mwaka wa pili) na Maria Soko (Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza).
Ndani ya gari hilo walikuwemo watu watano na mmoja kati yao ni Nkiko Bende mwanafunzi wa uhandisi wa viwanda mwaka wa tatu UDSM, aliyejeruhiwa na hivi sasa anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
“Wakati huu wa majonzi nawasihi wana jumuiya wote wa chuo kikuu kuwa watulivu na kuwaombea wanafamilia, ndugu na jamaa wa marehemu. Uongozi unatoa pole kwa msiba huu mkubwa na unamtakia afya njema na kumuombea apone haraka mwanafunzi aliyejeruhiwa,” amesema Profesa Anangisye katika taarifa hiyo.
Na Peter Godwin.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

WANAFUNZI, WATUMISHI WALIOFARIKI KWA AJALI KUAGWA KESHO NKURUMAH HALL
Reviewed by By News Reporter
on
6/13/2018 12:23:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: