Loading...

ATCL KUANZA SAFARI ZAKE NCHI ZA UGANDA NA BURUNDI

Loading...
KAMPUNI ya Ndege Tanzania (ATCL) imesema, ndani ya mwaka huu itakamilisha safari za ndege kwenda katika nchi za Afrika Mashariki, ikianza na Uganda na Burundi.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi katika mahojiano na gazeti moja hapa nchini hivi karibuni.
Alisema suala la kuchagua ruti ni la kimkakati, hivyo kampuni ina vigezo vinavyoiongoza katika kuchagua ruti, hivyo kampuni imeamua kwa sasa kuanza na nchi mbili za Afrika Mashariki ambazo ni Uganda na Burundi.
Kwa mujibu wa Matindi kampuni haitaingia sehemu huku ikijua kuwa inapata hasara, inaangalia vigezo ilivyojiwekea.
Matindi alisema kampuni imejiwekea Mpango Mkakati wa Miaka Mitano 2017 – 2022 ambapo ndani ya mpango huo kampuni inategemea kuwa na jumla ya ndege tisa zitakazofika kwa awamu tofauti.
NA Fatma Pembe.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
ATCL KUANZA SAFARI ZAKE NCHI ZA UGANDA NA BURUNDI ATCL KUANZA SAFARI ZAKE NCHI ZA UGANDA NA BURUNDI Reviewed by By News Reporter on 6/13/2018 11:47:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.