Loading...

HABARI ZA HIVI PUNDE: MSAFARA MWENYEKITI UVCCM TAIFA WAPATA AJALI MEATU

Loading...
Msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM, Kheri James wapata ajali wilayani Meatu baada ya gari la Polisi lililokuwa kwenye msafara huo limechomoka tairi.

Hakuna taarifa ya kifo lakini Majeruhi watatu wamekimbizwa katika hospitali ya Mwandoya kwa huduma ya afya na gari ya basi ya Rombo imepata ajali baada ya kuigonga gari ya madiwani kwa nyuma.

Ajali imetokea mpakani mwa wilaya za Meatu na Itilima katika kijiji cha Kisesa.
Wakuu wa wilaya za Meatu na Itilima wapo eneo la ajali kutoa msaada stahiki.

Msafara umeendelea baada ya majeruhi kufikishwa Mwandoya.

Shukrani zimwendee dereva wa basi la Rombo kwa kuchepusha gari nje ya barabara ili kulikwepa gari la polisi

Pia tunaishukuru Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ya Meatu kwa uharaka wake wa kulishughurikia tukio hili

Madiwani waliojeruhiwa ni kata za Imalaseko,Mwasengera na Ngoboko.
Na Geofrey Okechi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
HABARI ZA HIVI PUNDE: MSAFARA MWENYEKITI UVCCM TAIFA WAPATA AJALI MEATU HABARI ZA HIVI PUNDE: MSAFARA MWENYEKITI UVCCM TAIFA WAPATA AJALI MEATU Reviewed by By News Reporter on 6/10/2018 12:00:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.