Loading...

MBUNGE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI UGANDA

Loading...
Mbunge wa Manispaa ya Arua nchini Uganda,  Ibrahim Abiringa, mmoja wa waliokuwa mstari wa mbele kushinikiza mabadiliko ya Katiba ya Uganda ameuawa kwa kupigwa risasi juzi usiku.
Polisi imesema mwanasiasa huyo wa chama tawala cha National Resistence Movement (NRM) na mlinzi wake waliuawa karibu na makazi yake kaskazini mwa mji mkuu wa Kampala na watu wasiofahamika.

Rais Yoweri Museveni amesema kuwa amesikitishwa na mauaji hayo na kuagiza maofisa wa usalama kuwasaka waliomuua mbunge huyo.

Katika mtandao wake wa Twitter Museveni, alimuomboleza mbunge huyo akisema kuwa waliotekeleza kitendo hicho wana roho ngumu.

”Nimepokea habari kuhusu mauaji ya kinyama ya mbunge wa Manispaa ya Arua, Mheshimiwa Ibrahim Abiriga na mlinzi wake nje ya mji wa Kampala.

“Nimeviagiza vitengo vya usalama kuwasaka waliotekeleza kitendo hicho na taifa litajuzwa hivi karibuni”, aliandika Museveni.
Na Hamisi Fakhi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MBUNGE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI UGANDA MBUNGE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI UGANDA Reviewed by By News Reporter on 6/10/2018 10:41:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.