Loading...

MJUE PASTA ANAYETUMIA JOKA KUBWA KUTENDA MIUJIZA

Loading...
Kila Kukicha, mengi yanaibuka hasa katika maswala ya imani, wachungaji wakishindana kutoa mapepo na kufanya miujiza kwenye makanisa.

Watanzania wamekuwa wakishangaa wachungaji wa humu nchini kutokana na vitendo vya ajabu ajabu ambavyo huwafanyia waumini wao kwa misingi kuwa wanawapa uponyaji wa kiroho.

Sasa tukiangazia Afrika na dunia nzima kwa ujumla, Tanzania bado hajafikia maahabu yanayofanywa na wenzao na mataifa mengine.
Tukio la hivi karibuni lililomhusisha mhubiri kutoka Afrika Kusini, Lesego Daniel ambaye hufaamika kwa vituko vyake kwa wakati mmoja akiwalisha waumini wake nyasi na kuwanywesha petroli
Lesengo alifika madhabauni akiwa amebeba joka kubwa mkononi na kulitumia kufanya miujiza kwa waumini wake.
Kwa mujibu wa SDE, Daniel wa Rabboni Centre Ministry jijini Pretoria alionekana kutumia joka hilo kuhubiri kabla ya kuliweka mahali pa komunyo kuwagawia waumini wake.

Hili halikuwatisha kamwe waumini kwani walionekana kuwa na amani nyoka huyo akiwafanyia maajabu.
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MJUE PASTA ANAYETUMIA JOKA KUBWA KUTENDA MIUJIZA MJUE PASTA ANAYETUMIA JOKA KUBWA KUTENDA MIUJIZA Reviewed by By News Reporter on 6/10/2018 10:22:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.