Loading...

KOCHA JULIO ATAKA KUMSAJILI ALIKIBA KATIKA TIMU ZAKE

Loading...
Baada ya kumalizika kwa mechi ya kirafiki kati ya timu ya Alikiba na timu ya Mbwana Samatha ailiyofanyika uwanja wa taifa jumamozi iliyopita. kuekuwa na maoni mengi sana kuhusu mechi hiyo huku wakifurahi na kuwashukuru watu wote waliojitokeza kuangalia mechi hiyo iliyokuwa na lengo la kutumia pesa zilizopatikana kwa ajili ya kusaidia elimu katika shule zenye mazingira magumu.

Katika moja ya maoni yaliyojitokeza ni kuhusu Alikiba kutoka kwa kocha Jamhuri Kiwhelu maarufu kama 'Julio' aliyekuwa kocha kutoka upande wa Alikiba huku akisema kuwa msanii huyo ana uwezo mkubwa sana wa kucheza mpira lakini amekuwa akimshawishi kufanya mpira na amekuwa akimkatania kila mara.

"Mara nyingi nimekuwa nikimwambia alikiba aje nimsajili katika timu ninazofudisha ila hatokuwa akicheza mikoani mpaka timu itakapokuwa ikicheza dar es salaam ndio aje kucheza. Ninachoweza kusema ni kwamba alikiba ni mchezaji ambae akipata mwalimu anaejua kufundisha kama mimi anaweza kuwa mchezji mzuri sana."
Na Neema Joshua.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KOCHA JULIO ATAKA KUMSAJILI ALIKIBA KATIKA TIMU ZAKE KOCHA JULIO ATAKA KUMSAJILI ALIKIBA KATIKA TIMU ZAKE Reviewed by By News Reporter on 6/12/2018 07:45:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.