Loading...

MIMI NI MLEZI WA WASANII WOTE SIO WCB PEKEE - RC MAKONDA

Loading...
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam amefunguka na kusema kuwa yeye ni mlezi wa wasanii wote na sio WCB pekee kama watu wanavyodai lakini tu WCB walimfuata na kumuomba kuwasaidi kwa hilo. Akizungumza katika futari aliyoandaliwa  Mlimani City , Makonda amesema kuwa yeye amekuwa karibu na WCB kwasababu tu walimuomba lakini sio kwamba yeye sio mlezi wa wasanii wengine.

"Mimi ni mlezi wa wasanii wote lakini wasanii wanapokuomba kuwasiamamia kwa asilimia mia moja huo ni uamuizi wao tu,kwaio wao waliniomba mheshimiwa ebu tunaomba utuangalie na mimi nikasema haina shida kwa sabau waliamini wakiwa chini yangu wanaamini watafanya vizuri zaidi."

Kwa kipindi cha muda mrefu sasa, Mh Makonda amekuwa mlezi wa wasanii wa WCB na kuwa nao pamoja katika kufanya shughuli nyingi za kiamendeleo ya kijamii na muziki wao pia.
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MIMI NI MLEZI WA WASANII WOTE SIO WCB PEKEE - RC MAKONDA MIMI NI MLEZI WA WASANII WOTE SIO WCB PEKEE - RC MAKONDA Reviewed by By News Reporter on 6/12/2018 07:33:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.