Loading...

MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI WA DRC BEMBA AACHILIWA HURU

Loading...
Mahakama ya ICC imemuachilia huru makamu wa rais wa zamani wa nchini DRC Jean Pierre Bemba baada ya mahakama hiypo kumuondolea makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu ambayo alikuwa amepatikana nayo.

Alikuwa anatumikia kifungo cha miaka 18 jela kutokana na makosa hayo.

Bemba alipatikana na hatia mwezi Machi mwaka 2016 kwa makosa ya uhalifu, uliotokea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003 na akahukumiwa 21 Juni.

Mahakama hiyo imetoa uamuzi huo kufuatia rufaa aliyoiwasilisha kupinga hukumu hiyo.

Bemba ambaye alipoteza kinyang'anyiro cha kuwania urais nchini DR Congo 2006 anatarajiwa kuunganishwa na mkewe na wanawae wanaoishi nchini Ubelgiji.

Kuna uvumi kwamba huenda akawania urais katika uchaguzi wa urais nchini DR Congo mnamo mweiz Disemba

Uamuzi wa mahakama umepokelewa kwa shangwe na wafuasi wake waliokuwepo ukumbi wa mahakama, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Alilaumiwa kwa kushindwa kuwazuia waasi wake wasiwaue na kuwabaka watu.

Jaji leo amesema mwanasiasa huyo hawezi kulaumiwa kwa vitendo vya waasi hao.

Jaji Christine Van den Wijngaert pia amesema majaji waliomhukumu mwaka 2016 walikosa kuzingatia juhudi zake za kujaribu kuzuia uhalifu huo punde baada yake kufahamishwa kwamba makosa hayo yalikuwa yakitokea.

Kesi hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa ICC kuangazia ubakaji kama silaha wakati wa vita.

Aidha, ilikuwa mara ya kwanza kwa mshtakiwa kuhukumiwa kwa makosa yaliyotekelezwa na watu wengine waliokuwa chini ya mamlaka yake.

Reuters wanasema Bemba anatarajiwa kuendelea kuzuiliwa huku uamuzi ukisubiriwa kuhusu rufaa ya kesi dhidi yake ya kukaidi uamuzi wa mahakama.

Baadhi ya wafuasi wa Bemba walikusanyika kufuatilia uamuzi wa mahakama kupitia runinga Kinshasa

Akitoa hukumu mwaka 2016, Jaji Sylvia Steiner alikuwa amesema kuwa Bemba alishindwa kudhibiti waasi wake ambao walitumwa kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Bemba alikuwa ametuma zaidi ya wapiganaji 1,000 kwenda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kumsaidia rais wa zamani Ange Felix Patasse, kukubiliana na jaribio la mapinduzi.
Na Paskali Joseph.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI WA DRC BEMBA AACHILIWA HURU MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI WA DRC BEMBA AACHILIWA HURU Reviewed by By News Reporter on 6/13/2018 09:00:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.