Loading...

MKE WA PASTA ADANGANYA KUTEKWA KISA MILIONI 29

Loading...
Mariam Kusuubira alidanganya umma, mumewe pasta Shadrack wa kanisa la Noah's Ark wa Masija Uganda kuwa alikuwa ametekwa nyara na waliomteka walihitaji Milioni 29, pesa za Kitanzania ili kumuachia huru.

Kulingana na msemaji wa polisi mjini Kampala Luke Owoyesigyre, Miriam alitoa ujumbe wa uongo akidai alitekwa nyara.

Alidai alitekwa na watu wasiojulikana Juni 6, 2018 alipokuwa njiani kuelekea kununua shamba.

Pasta ambaye hangeweza kutoa hela hizo aliripoti kisa hicho kwa polisi akihofia usalama wa mkewe.

Baada ya msako mkali, maafisa hao wa polisi walimpata mkewe pasta akiwa amejificha katika nyumba ya mwanaye wa kike na mpaka sasa haikubainika kwanini Mariam alihitaji pesa hizo.
Na Neema Joshua.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MKE WA PASTA ADANGANYA KUTEKWA KISA MILIONI 29 MKE WA PASTA ADANGANYA KUTEKWA KISA MILIONI 29 Reviewed by By News Reporter on 6/13/2018 09:23:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.