Loading...

MAMA HAMISA APATA KIGUGUMIZI DIAMOND KUMPA BINTI YAKE UJAUZITO TENA

Loading...
Wakati habari za ‘ujauzito mpya’ wa Hamisa Mobetto zikizidi kushika kasi kwenye mitandao ya kijamii, mama yake amegoma kuthibitisha akisema hana muda wa kujibu taarifa za mitandaoni.

Akizungumza na Mtandao mmoja wa hapa nchini, Mama Hamisa amesema habari ya ujauzito amezisikia katika mitandao na kwamba kama kweli binti yake ana ujauzito basi hilo ni jambo la kheri.

"Unajua mimi sipendi sana kuongea ongea na sio kama siwezi ila najijua mimi mtu wa Musoma huwa nakuwa na hasira za karibu sana, ndio maana mambo mengi yanayotokea mitandaoni huwa nakaa kimya ili kulinda heshima yangu.
"Mfano hiyo ishu ya Hamisa kuwa mjamzito mimi nimeisikia mitandaoni na kama kweli mimi sioni tatizo, hilo ni jambo la kheri kwetu," alisema Mama Hamisa.

Hamisa anadaiwa kuwa na ujauzito wa miezi mitatu wa mwanamuziki Diamond ambaye pia ni baba wa mtoto wake wa pili Daylan.

Mwanamitindo huyo pia ana mtoto mwingine wa kike aliyezaa na mmiliki wa kituo cha redio na televisheni cha EFM na ETV, Dj Majizzo.
Na Neema Joshua.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MAMA HAMISA APATA KIGUGUMIZI DIAMOND KUMPA BINTI YAKE UJAUZITO TENA MAMA HAMISA APATA KIGUGUMIZI DIAMOND KUMPA BINTI YAKE UJAUZITO TENA Reviewed by By News Reporter on 6/05/2018 06:33:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.