Loading...

'MAYATIMA NI BUSARA KULELE KATIKA FAMILIA ZAO'

Loading...
MKURUGENZI Mtendaji wa taasisi ya TAQWA Tanzania, inayotowa misaada kwa watoto mayatima, Dk. Salha Mohamed Kassim amewataka waumini wa dini ya kiislamu nchini, kuwalea watoto mayatima ndani ya familia zao na sio kuwapeleka katika vituo vya kulelea mayatima baada ya kufiliwa na mzazi wao.

Dk.Salha alitowa wito huo skuli ya Ole, baada ya kukabidhi futari kwa watoto mayarima waliopo chini ya Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran na Maendeleo ya Kiislamu ya Ole, ambapo zaidi ya kaya 456 kutoka Ole na Kiungoni zimepatiwa futari.

Alisema watoto mayatima wanapaswa kulelewa na jamaa zao wa karibu, ili wapate mapenzi kutoka kwao na sio kuwapeleka katika sehemu za kulelewa.

Alisema waislamu wanapaswa kufuata vigezo vya Mtume Muhammad (S.A.W), kwani yeye alipofiliwa na babaake alelewa jamaa zake wa karibu, hivyo jamii nayo inapaswa kufahamu na kufuata nyayo hizoo.

“Sisi tunamfuata historia ya Bwana Mtume (S.A.W) yeye alizaliwa yatima, alilelewa na babu yake kasha akalelewa na ami yake, yote ni kuonesha alipata mapenzi kutoka kwa familia yake”alisema.

Aidha alizipongeza familia zote zinazolea watoto mayatima majumbani mwao, kwani watoto hao wanahitaji huduma nyingi muhimu kutoka kwa wazazi.

Akizungumzia kuhusu TAQWA alisema taasisi hiyo ilianza mwaka 2011 baada ya kutokea matihani wa meli, hadi sasa inaendelea kusaidia watoto mayatima.

Alisema kwa sasa taasisi hiyo imepanga kwa mwaka huu 2018 kuzifikia kaya 1000, kwa kuzipatia futari Tanzania nzima, tayari imeshaanza na Kisarawe, Mkurunga, Dar es Salam, Morogoro na Pemba.

“Bado tunaendelea kuwataka waislamu na wasio kuwa waislamu kusaidia, kuunganisha nguvu zao kwa kutoa misaada yao kwani watoto mayatima wanahitaji kujiona wako sawa kama watoto wengine”alisema.

Shekhe Salum Juma kutoka jumuiya ya tahfidhi QURAN na maendeleo ya Kiislamu Ole, aliipongeza TAQWA kwa kuendelea kuwa saidia mayatima kila mwaka unapofika.

Alisema watoto mayatima wanapopatiwa misaada kama hiyo hujiona wako vizuri sawa na watoto wasiokua mayatima, hivyo jamii inapaswa kuwaona mayatima kwa hali na mali katika kuwasaiida.

Kwa upande wao wanafamilia wanaolea watoto mayatima, wameipongeza taasisi ya TAQWA kwa kuwasaidia mayatima Kisiwani Pemba, sambamba na kuwaomba wahisani kusaidia juhudi hizo zilizoanzishwa na TAQWA.

Huo ni mwaka wa saba kwa Taasisi ya TAQWA, kutowa msaada wa vyakula kwa wa watoto mayatima kisiwani Pemba, kila ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Na Mohamedi Makame.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
'MAYATIMA NI BUSARA KULELE KATIKA FAMILIA ZAO' 'MAYATIMA NI BUSARA KULELE KATIKA FAMILIA ZAO' Reviewed by By News Reporter on 6/08/2018 08:02:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.