Loading...
MOTO mkubwa umeteketeza jengo la utawala la Shule ya Sekondari Kazima katika Manispaa ya Tabora na kusababisha uharibifu mkubwa wa nyaraka mbalimbali ikiwemo mitihani ya kujipima ya kidato cha nne na cha tano.
Akizungumza na wanahabari Mkuu wa Shule hiyo Mrisho Kivuruga, amesema jengo hilo limeanza kuungua na moto majira ya saa tisa usiku wa kuamkia leo Jumamosi na kuteketeza nyaraka zote muhimu za shule hiyo ikiwemo vyeti vya wanafunzi, mitihani ya kujipima uwezo iliyomalizika juzi, chumba cha zahanati, vitabu na vifaa mbalimbali vilivyokuwemo katika jengo hilo na ofisi zake zote.
Naye Ofisa Elimu Mkoa wa Tabora Suzan Nyarubamba amesema, kufuatia kuteketea mitihani hiyo uongozi wa Mkoa utasimamia ili wanafunzi hao warudie mitihani yao
Na Peter Godwin.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

MOTO MKUBWA WATEKETEZA SHULE TABORA
Reviewed by By News Reporter
on
6/02/2018 11:14:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: