Loading...

YANGA YANYAKUA KIFAA KUTOKA BENIN KUZIBA PENGO LA NGOMA

Loading...
YANGA ni kama imejibu mashambulizi baada ya juzi usiku kumshusha msham­buliaji wa timu ya Taifa ya Benin na Klabu ya Buffles du Borgou FC ya nchini huko, Marce­lin Degnon Koukpo na jana usiku alitarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili.

Vigogo wa Yanga wam­emshusha mchezaji huyo ambaye inadaiwa kwamba ndiye mbadala wa Amissi Tambwe ambaye inaoneka­na maji yamezidi unga na huenda wakaachana nae kama ilivyokuwa kwa Don­ald Ngoma aliyetua Azam kwa Hans van Der Pluijm.

Tambwe alikuwa akiwa­kosha Yanga kutokana na uwezo wake wa kutupia hata kwa vichwa ambavyo Mbenin huyo amewaambia viongozi kwamba hiyo ni kazi ndogo kwake kwani amekuwa akiifanya marany­ingi.

Marcelin alitua nchini juzi Alhamisi usiku akitokea kwao Benin kwa ajili ya kumalizana na Yanga akiwa kama mchezaji huru na kama mambo yamekwenda sawa jana huu utakuwa ndiyo usajili wa kwanza wa Kocha Mkongomani, Mwinyi Zahera.

Mbenin huyo mwenye mi­aka 23, tofauti na uwezo wa kupiga vichwa, pia viongozi wa Yanga wanadai wameam­biwa na kocha kwamba ana uwezo wa kupiga mashuti ya mita 20.

Yanga ambayo bado haijaimarika kiuchumi, inafanya maboresho katika safu ya ushambuliaji haswa kutokana na kuwepo kwa uwezekano wa Mzambia, Obrey Chirwa kuibukia Simba kuchukua nafasi ya Laudit Mavugo ambaye ameshaam­biwa kwamba hana chake.
Na Hamisi Fakhi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
YANGA YANYAKUA KIFAA KUTOKA BENIN KUZIBA PENGO LA NGOMA YANGA YANYAKUA KIFAA KUTOKA BENIN KUZIBA PENGO LA NGOMA Reviewed by By News Reporter on 6/02/2018 11:08:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.