Loading...

NDALICHAKO AMUAMBA WAZIRI MWALIMU KWASAIDIA PACHA WENGINE WALIOUNGANA

Loading...
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Joyce Ndalichako amemuomba Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuwasaidia watoto wengine pacha walioungana kama walivyokuwa Maria na Consolata.

Profesa Ndalichako ameyasema hayo jana Juni 6 katika mazishi ya pacha walioungana, Maria na Consolata Mwakikuti, yaliyofanyika, Iringa.

Amesema kila mtoto amezaliwa kwa namna yake hivyo kuwasaidia kutawafanya wakue vizuri kama ilivyo kwa Maria na Consolata.

“Ni wakati kwa jamii kutokubali kuwaficha watu wenye ulemavu kwa kuwa wakipewa maarifa wanaweza kufanya mambo makubwa,” amesema
Pacha wengine wenye umri wa miezi mitano, wapo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili walikohamishiwa wakitokea, Kituo cha Afya cha Misenyi, Kagera.
Na Paskali Joseph.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
NDALICHAKO AMUAMBA WAZIRI MWALIMU KWASAIDIA PACHA WENGINE WALIOUNGANA NDALICHAKO AMUAMBA WAZIRI MWALIMU KWASAIDIA PACHA WENGINE WALIOUNGANA Reviewed by By News Reporter on 6/07/2018 10:19:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.