Loading...

PIERRE NKURUNZIZA: SINTOWANIA MUHULA MWINGINE KATIKA UCHAGUZI WA URAIS WA MWAKA 2020

Loading...
Wakati wa sherehe rasmi ya utiaji sahihi kwenye Katiba mpya ya Burundi, Rais Pierre Nkurunziza ametangaza kwamba hatowania muhula mwengine katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Sherehe ya utiaji sahihi imefanyika Alhamisi wiki hii katika ikulu ya rais mjini Gitega, katikati mwa Burundi.

Hatua hii itafuatiwa na zoezi la kuitambulisha Katiba hii mpya. Zoezi ambalo litaanzia wilayani Bugendana, mkoani Gitega, ambapo Rais Nkurunziza anaelekea kuitambulisha kwa wakaazi wa wilaya hiyo.

Bugendana ndiko kulikozinduliwa rasmi mchakato wa katiba, lakini pia kampeni ya chama madarakani CN DD/FDD ya kuipiga debe katiba hiyo.

Kwa upande wa upinzani, kupitishwa kwa Katiba hii mpya kumefuta mkataba wa Amani wa Arusha uliosainiwa mwaka 2000, ambao uliweka utaratibu wa kugawana madaraka kati ya makabila nchini humo.

Katiba hiyo mpya imeongeza muhula wa urais kutoka miaka mitano hadi saba.

Upinzani unasema kuwa katiba hiyo mpya inampa Rais Nkurunziza ambaye alitawazwa na chama chake cha CNDD-FDD 'Kiongozi wa Milele’ mapema mwaka 2018, kuvunja sheria anavyotaka bila kikwazo.

Katiba hii mpya ambayo inaanza kutekelezwa Alhamis wiki hii itageuza mambo mengi kwenye taasisi za maongozi ya taifa.

Katiba hii pia inaanza kutekelezwa wakati mazungumzo ya amani yakiwa yamekwama baada ya serikali kukata kuketi meza moja na wapinzani. Kufuatia hali hiyo ya mkwamo,

Nkurunziza, 54, amekuwa mamlakani tangu 2005. Utawala wake umekumbwa na misukosuko tangu 2015 baada ya kupuuzilia mbali mkataba wa kutowania urais tena.
Na Hamisi Fakhi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
PIERRE NKURUNZIZA: SINTOWANIA MUHULA MWINGINE KATIKA UCHAGUZI WA URAIS WA MWAKA 2020 PIERRE NKURUNZIZA: SINTOWANIA MUHULA MWINGINE KATIKA UCHAGUZI WA URAIS WA MWAKA 2020 Reviewed by By News Reporter on 6/08/2018 09:03:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.