Loading...

POLISI WAFANYA MSAKO MATAPELI WA MESEJI ZA SIMU

Loading...
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kitengo cha upelelezi wa makosa ya mtandaoni, (Cybercrime investigation unit) kinafanya uchunguzi kuwabaini wanaotuma ujumbe mfupi wa simu za mkononi kwa nia ya kuwatapeli wananchi.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Barnabas Mwakalukwa, juzi Juni 6, imesema yeyote aliyetapeliwa anatakiwa kutoa taarifa kwani jumbe hizo zina lengo la kuwatapeli na kuwaibia fedha wananchi.

“Tunawataka wananchi kuacha kutumia simu na mitandao ya kijamii vibaya na badala yake itumike kuhabarisha na kuelimisha jamii juu ya mambo mbalimbali ya maendeleo,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema, baadhi ya jumbe hizo ni zile zinazosema. ‘Ile hela tuma kwa namba hii’ au ‘usipige kwa sasa, spika imeharibika, tuma ujumbe,’ au ‘Mjukuu wangu ile ndagu niliyokutumia imefanya kazi na sasa unapata wateja wengi… sasa njoo uchukue ndagu nyingine ya mvuto.’
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
POLISI WAFANYA MSAKO MATAPELI WA MESEJI ZA SIMU POLISI WAFANYA MSAKO MATAPELI WA MESEJI ZA SIMU Reviewed by By News Reporter on 6/08/2018 05:25:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.