Loading...

VISA VYA UTEKAJI NYARA KWA WATOTO VYAKITHIRI KIVU KUSINI

Loading...
Kuanzia mwezi Januari 2017 hadi mwezi Mei 2018, karibu watoto 85 walitekwa nyara katika mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. viongozi tawala katika mkoa huo wamethibitisha hali hiyo.

Mashirika ya haki za binadamu yameiomba serikali kukomesha hali hii, ambayo inachingia kwa mdororo wa usalama nchini.

Kiongozi wa shirika la haki za binadmu la ASADHO, Joshua Blaise Mukubwa, anasema hali hii inatisha, huku akiwalamu viongozi wa mkoa wa Kivu Kusini kushindwa kudhibiti hali hii.

Kwa mujibu wa Bw Mukubwa maeneo ya pwani ya mkoa wa Kivu Kusini, karibu na Ziwa Kivu na Ziwa Tanganyika, ni maeneo yaalioathirika zaidi na visa hivi vya utekaji nyara kwa watoto ambavyo vilianza kuongezeka tangu mwanzoni mwa mwaka 2018.

Wakati huo huo Idara ya uhamiaji nchini DRC imechukua hatua kwa mtu yeyote anayetaka kuvuka mpaka na mtoto mdogo.
Na Fatma Pembe.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VISA VYA UTEKAJI NYARA KWA WATOTO VYAKITHIRI KIVU KUSINI VISA VYA UTEKAJI NYARA KWA WATOTO VYAKITHIRI KIVU KUSINI Reviewed by By News Reporter on 6/08/2018 05:49:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.