Loading...

RAMOS HATIMAYE AVUNJA UKIMYA NA KUFUNGUKA KUMUUMIZA MO SALAH

Loading...
BEKI na Nahodha wa Real Madrid ya Hispani, Sergio Ramos amesema hatua ya Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah kumshika mkono kwanza ndiyo iliyosababisha mchezaji huyo kuumia wakati wa Fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wiki chache zilizopita.

Salah (25), alitoka uwanjani akitokwa na machozi huku akiacha mechi ikiendelea baada ya kuumia begani na baadaye alifanyiwa upasuaji.

Mhispania Ramos pia aligongana na Kipa wa Liverpool, Loris Karius ambaye inadaiwa alipata jeraha kwenye ubongo kabla ya hajafanya makosa mawili yaliyochangia kufungwa na Madrid bao 3-1 kwenye mechi hiyo iliyochezewa Kiev, Ukraine.

Ramos anafunguka;

“Kitu pekee ambacho sijakisikia ni Roberto Firmino akisema kwamba alipata mafua kwa sababu aliangukiwa na jasho langu, (amesema Ramos kwa utani), iwapo Salah angedungwa sindano kipindi cha pili angeendelea kucheza mechi hiyo.

“Upuuzi mtupu, wamemzungumzia sana Mo Salah, mimi sikutaka kuzungumza kwa sababu kila kitu kimeongezwa chumvi.

“Nautazama mchezo vyema, anaushika mkono wangu kwanza na ninaanguka upande mmoja, na jeraha lilitokea kwenye mkono ule mwingine. Wanasema kwamba nilishika mkono na kuukatalia kama mchezaji wa judo, kipa wao anasema nilimduwaza kwa kumgonga,” amesema Ramos.

“Niliwasiliana na Salah kupitia ujumbe, alikuwa anaendelea vyema. Nimefanya hivyo mara kadha lakini wakati ni Ramos anapofanya jambo kama hilo, linasemwa zaidi.

“Sijui kama ni kwa sababu nimekuwa Madrid kwa muda mrefu na nimeshinda vikombe kwa muda mrefu sana kiasi kwamba watu hunitazama tofauti.”

Licha ya Salah kuumia, ametajwa kwenye kikosi cha Misri kitakachocheza Kombe la Dunia nchini Urusi. Inaaminika kwamba huenda akashindwa kucheza mechi yake za kwanza Urusi, lakini atashiriki mechi za baadaye.

Wengi wa mashabiki wa Liverpool wanamlaumu Ramos kutokana na kuumia kwa Salah, tukio ambalo mwamuzi hakutoa adhabu yooyte. Ombi limeanzishwa kuwataka Fifa na Uefa kumwadhibu mchezaji huyo wa Uhispania.

Wakili mmoja nchini Misri amewasilisha kesi ya kutaka Ramos atakiwe kulipa fidia ya £874m kwa madhara na hasara aliyowasababishia raia wa Misri “kimwili na kiakili.” Makosa mawili ya Karius yaliwasaidia Real kushinda na madaktari Marekani wamesema huenda kugongana kwake na Ramos kuliathiri uchezaji wake.
Na Hamisi Fakhi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RAMOS HATIMAYE AVUNJA UKIMYA NA KUFUNGUKA KUMUUMIZA MO SALAH RAMOS HATIMAYE AVUNJA UKIMYA NA KUFUNGUKA KUMUUMIZA MO SALAH Reviewed by By News Reporter on 6/07/2018 11:28:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.